1. Kwa salama Baba Mungu Awalinda watu wake.
Hata nyota za mbinguni, Si salama kama wao.
2. Mungu awalinda hivyo Katika upendo wake.
Wanakumbatiwa naye,Wanarehemiwa sana.
3. Hawavutwi toka kwake Kwa furaha wala shida.
Yeye ni rafiki mkubwa, Kwa walio watu wake
4. Wanalishwa wanavikwa, Wanafarijiwa naye.
Hata nywele za kichwani, Zimehesabiwa zote.
5. Enyi kundi lake dogo, Mungu atawahifadhi! Na
adui watashindwa Kwa uwezo wake mwingi.
6. Akitoa, akiwapa, Baba yetu hageuki. Na
mapenzi yake ndiyo, Watoto wapate mema.
Comments
Post a Comment