1. Mikononi mwa Yesu, nalindwa salama.
Mchunga wangu mwema,Yeye ananipenda,
Hapa ninasikia, ‘Toka mbinguni juu,
Nyimbo za malaika, wam-sifu Mungu.
Mikononi mwa Yesu Nalindwa salama.
M-chunga wangu mwema, Yeye ananipenda.
2. Mikononi mwa Yesu, Mbali na huzuni,
Dhambi na majaribu, Mungu ni ngome
yangu, Mawimbi na tufani, Zinatulia hapa. Sasa
muda kitambo Nafika bandarini.
3. Yesu Mwokozi wangu, Ulinifilia. Juu ya
mwamba Kristo, ndipo napum-zika. Usiku
utapita, Mwanga wa alfajiri,
Utanikuta mle, Nyumbani mwa Mungu.
Comments
Post a Comment