55 TUPATE KWA NANI FARAJA YETU?


1. Tupate kwa nani faraja yetu?
Kwa Yesu, kwa Bwana Yesu.
Msingi wa kuendelea wapi?
Kwa Yesu, kwa Bwana Yesu.


Kwa Yesu, kwa Yesu, Ninashangalia rohoni
mwangu.Uheri wa huko haufasiriwi Moyoni
naufahamu.


2. Maji ya uzima nipate wapi?
Kwa Yesu, kwa Bwana Yesu.
Chakula nyikani kiko kwa nani?
Kwa Yesu, kwa Bwana Yesu.


3. Mahali pa kustarehe ni wapi?
Kwa Yesu, kwa Bwana Yesu.
Na nguvu ya kuendelea mbele?
Kwa Yesu, kwa Bwana Yesu.


4. Ni nani abatizaye kwa Roho?
Ni Yesu, ni Bwana Yesu.
Pendo la udugu ’toka kwa nani?
Kwa Yesu, kwa Bwana Yesu.


5. Wakristo watakusanyika wapi?
Kwa Yesu, kwake mbinguni.
Watashangilia milele huko,
Kwa ’jili ya pendo lake.


Comments