57 YESU KWA UPENDO ULINIFILIA


1. Yesu, kwa upendo ulinifilia. Nivute karibu
nawe zaidi. Nijaze moyoni upendo wako mkuu,
Niwe tayari tu Kuwa dhabihu.


2. Wewe uliye juu unaniombea, Ili nikubali
mapenzi yako, Nibebe msalaba hata kwa
furaha. Nipe ujasiri Kuwa shahidi.


3. Roho wako Bwana awe ndani yangu,
Nikutumikie maisha yote. Niwe m-fariji kwa
wenye huzuni, Niwavute kwako walio mbali


4. Vipawa ninavyo vimetoka kwako. Vipokee
Bwana kama sadaka. Kule mbinguni juu nitaona
ukuu wako,Yesu wangu, U yote kwangu!


Comments