1. Unipe raha tele kama mto,
Nipite jangwani kwa furaha.
Unipe na imani tena, Yesu,
Ningoje siku yako kwa subira!
2. Kwa siku chache ninaona shida,
Dhoruba zinanisumbua huku.
Napanda mbegu zangu nikilia,
Lakini nitavuna kwa furaha.
3. Kwa siku chache ninaburudishwa,
Nikionja maji ya uzima.
Lakini siku moja nitakunywa,
Maji katika kisima chenyewe.
4. Kwa siku chache naitunza taa,
Nadumu kukesha na kuomba.
Na siku za uchungu ziishapo,
Nitamkuta Yesu huko juu.
Comments
Post a Comment