1. Yesu ninakutolea moyo na Mwili wangu,
Niwe mfuasi wako, Safi m-takatifu!
Ee Yesu, Mwokozi
Nitakase saa hii!
2. Ee Mwokozi , nitakase, Unijaze upendo.
Na maisha yangu yote, yawe yako, Bwanangu!
3. Napenda kukuheshimu, Wewe Mwokozi wangu.
Nifanane nawe Yesu, Mbele ya watu wote!
4. Ninakaa kusikiliza, Kama Yule Maria,
Nifundishe nawe Yesu, Ili nisipotee!
5. Mimi tawi ndani yako, Wewe u Mzabibu.
Nitakaswe nawe Bwana, Nikazae matunda!
Comments
Post a Comment