Skip to main content
- Twamsifu Mungu daima, Kwa damu takatifu,
Inayotosha kutoa, Makosa yetu yote.
- Wakristo wakusanyika, Karibu na kisima,
Hawapungukiwi kitu, Wakaa kwa Mwokozi.
- Tuimbe ulimwenguni, Juu ya upendo wake,
Kwa kuwa twafunguliwa, Kisima cha Golgotha.
- Yesu Kristo ni kisima, Cha maji ya uzima,
Wenye shida wastarehe, Waburudishwa kweli.
- Wenye dhambi wanaitwa, Kwa wingi wa
rehema,Wakosaji na maskini, Wasaidiwa sana.
- Tumepata tunu kubwa, Neema kwa neema!
Atakayeipokea, Ni mtu wa uheri.
- Haleluya! Twam-sifu Mwenyezi, Na Mwanawe
Na Roho M-takatifu, Haleluya! Amina.
Comments
Post a Comment