1. Ni heri kuona ndugu, tunapokwenda
mbinguni, Tukinyong’onyea sana, kwa
kuwa tu peke yetu.Kushirikiana kwa
ndugu, Kunatuburidisha, Na Mungu
atupa nguvu, Tukimwinulia macho.
2. Twafungamana rohoni, Tulio wa nyumba
Yake. Hakuna mfano wake, Kushirikiana
kwetu. Na tuna Mwokozi mmoja, Imani
moja pia, Watoto wa Baba mmoja,
Twashika sheria yake.
3. Furaha ya ulimwengu, Kitambo inatoweka,
Dhambi na fahari yake, hazitatuvuta tena. Lakini
tukikusanyika, Kwa jina la Yesu tu, Atuandalia
kweli, Karamu iliyo bora.
4. Tukivumilia hata, Ukomo wa mashindano,
Mbinguni tutawaona, Wakristo wapenzi wote.
Na huko hatutaachana, Tutakuwa pamoja.
Milele tutafurahi, Nyumbani mwa Baba yetu.
Comments
Post a Comment