1. Mungu univute, Nije kwako katika mateso,
shida na yote. Safarini mwote wimbo wangu
uwe; “Mungu univute karibu nawe!”
3. Bwana nionyeshe Njia yako, Yote nipokee
Kutoka kwako. Kifuani mwako, Unipe faraja,
Mungu univute, Karibu nawe!
4. Kwa ’jili ya yote, Nashukuru, Nikijaribiwa,
Nikukumbuke. Na katika yote, Ombi langu liwe:
“Mungu univute, Karibu nawe!”
5. Jua likishuka, Maishani, Niko peke yangu,
Katika giza. Baba nakuomba: “Nikukaribie,
Mungu, univute Karibu nawe!”
6. Nitakapoacha, Dunia hii, Kuitika mwito,
Kwenda mbinguni, Nitaimba tena, Na
watakatifu: “Mungu tumevutwa, Karibu nawe!”
Comments
Post a Comment