63 YESU MWOKOZI UNIVUTE


1. Yesu Mwokozi, univute Karibu nawe,
unifariji. Na kifuani mwako, Yesu
:/: Unipe raha na utulivu!:/:


2. Yesu Mwokozi, univute, mimi maskini,
unikubali. Sina chochote ila dhambi
:/: Kwa damu yako unisafishe!:/:


3. Yesu Mwokozi, niwe wako, Niondolee
hatia zote. Kwako, Ee Bwana, nina raha.
:/: Hata milele nikae nawe!:/:


4. Yesu Mwokozi, univute, Hata nifike
mbinguni kwako. Huko milele nitaimba.
:/: Shukrani na sifa zangu kwako:/:


Comments