64 KIMYA, EE MOYO WANGU


1. Kimya, Ee moyo wangu, Karibu na Yesu!
Huko inakupasa kubaki daima.
Njia salama ipi huku duniani,
Ukimwacha Yesu hata Neno lake?


Ushike mkono wangu, Bwana nakuomba!
Uniongoze njia, Nifike mbinguni!


2. Kimya, Ee moyo wangu, Omba kwa imani!
Nuru itatokea, Umwamini Mungu!
Na umwambie Yesu shaka zako zote.
Akuonyeshe njia, Na akutakase.


3. Kimya, Ee moyo wangu, shika Neno lake!
Lakuletea nguvu, Hekima ‘toka juu.
Na ukiendelea Katika kulitii,
Mungu atakujaza Nguvu na ushindi.


Comments