65 JU-U YA NYOTA ZOTE


1. Ju-u ya nyota zote Kuna nchi nzuri, Mji
wake ni Yerusalem’; Hakuna dhambi huko,
Wala shida na kufa, Na humo ninapenda kukaa.


Huzuni na machozi Hayatakuwako huko,
Wala unyonge au majaribu. Na hatutaumizwa
na mambo ya dunia Mjini mwa Yerusalemu.


2. Nitakapoingia, Nitamwona Mwokozi,
Ambaye alinifilia. Na nitam-shukuru Huyu
Mwana wa Mungu, Ndiye aliyenikomboa.


3. Huko nitawaona Mashujaa wa Biblia,
Walioshinda kwa imani. Pamoja nao wote,
Nitam-sifu Mungu Ju-u ya ne-ema yake kuu.


Comments