66 WATAKATIFU WOTE


1. Watakatifu wote Kutoka nchi zote,
Watakutana kwa Bwana Yesu, Kati’ ufalme
wake, Kuona uso wake, Na kujazwa uheri.
Wataimba milele pamoja na Bwana.


Watoka mashariki, Watoka magharibi,
Watoka popote duniani, Wanafika kwa
Mungu. Wenye mavazi safi, Watamwona
Mwokozi, Aliyewafilia juu ya msalaba.


2. Waliokombolewa Watakuwa pamoja,
Hakuna dhambi na shida tena
Mbinguni kwa Mwokozi. Ya kale
yamepita, Mambo yote ni mapya,
Itakuwa raha tu pamoja na Yesu.


3. Mlango wa ne-ema, U wazi hata kwako.
Yesu aita: “Njo-oni kwangu,
Nafasi ingaliko!” Waliotangulia
watungojea huko, Nyimbo za malaika
zatukaribisha.


Comments