1. Tunakaribia kao la mbinguni, Hata jua
likifichwa winguni. Tumfuate Bwana Yesu
siku zote. Kushiriki naye ni furaha kuu.
Twakaribia kufika mbinguni, haleluya!
Asifiwe! Jipe moyo safarini kwa kuwa
Mwokozi yu pamoja nasi!
2. Tunakaribia kao la mbinguni, Hata kwenye
dhoruba na upepo. Bwana Yesu yupo na
uwezo wake, Hatarini tutam-tegemea.
3. Njia yetu inapita kwenye jangwa, Mara nyingi
migu-u twaumizwa. Walakini tunakwenda
tukiimba, Twamsifu, Yesu, Mwokozi wetu.
4. Mwendo wetu utaisha siku moja, Tutapata
kustarehe huko juu. Tukiona shaka, shida
hapa chini, Utulivu tutapata kwa Yesu.
5. Twakaribia kufika mbinguni, haleluya!
Asifiwe! Tumelikaribia lengo letu,
Njoo ndugu yangu, twende sote!
Comments
Post a Comment