68 MBINGUNI KWA MKOMBOZI WANGU


1. Mbinguni kwa Mkombozi wangu,
Nami nitawasili siku moja. Na nitayaona
makovu yake, Sauti yake nitaisikia.


2. Makao ya milele tayari, Mwokozi
aliyotuandalia. Huko tutam-sifu sana
Yesu, Aliyetuokoa na hatari.


3. Na nyimbo za wokovu zaimbwa, Mbinguni
mbele ya Mwokozi wetu. Ukisikia habari
za huko, Vitani tunapata ushujaa.


4. Yesu kristo yupo nasi leo, Katika giza
atumulikia. Na neno lake ni upanga wetu,
Ahadi na safina juu ya maji.


5. Tukeshe, tukimngojea Yesu! Twakaribia
mwisho wa safari. Tuingojee asubuhi ile,
Atatukaribisha Bwana Yesu.


Comments