1. Je, tutaonana tena, Huko ng’ambo ya Yordan’
Na pamoja na Wakristo, Kuingia rahani?
Twonane, Twonane, Huko ng’ambo ya
Bahari! Tuonane kwa furaha, Huko hakuna shida.
2. Je, tutaonana tena, Baada ya dhoruba.
Huko katika bandari, Ya salama na raha?
3. Je, tutaonana tena, Na kum-sifu Mungu,
Pamoja nao wengine, Waimbao huko juu?
4. Waliotuacha huku, Tutaonana nao;Je,
tutawaona wote, Kwenye makao mema?
5. Tutamwona Bwana Yesu Kutanoni huko
juu,Tutakaribishwa naye Katika karamu kuu.
Comments
Post a Comment