7 MWOKOZI AMETIMIZA WOKOVU

  1. Mwokozi ametimiza wokovu,
    Kwa neema kubwa, Na juu ya mwamba wa
    Neno lake, Najenga imani.


    Aliniokoa kabisa! Kwa damu ya aliniosha.
    Ninam-shukuru Mwokozi m-pendwa,
    Kweli alinikomboa.



  2. Mzigo wa dhambi aliondoa,
    Kwa neema kubwa, Naona furaha,
    Rohoni mwangu, Amani ya Mungu.


  3. Naweza kukaa safi rohoni,
    Kwa neema kubwa, Na Roho
    wa Mungu aniongoza, Njiani daima.


  4. Karibu na Yesu niko salama,
    Kwa neema kubwa, Ahadi
    za Mungu zanipa raha, Iliyo kamili.

Comments