70 BARAGUMU LITALIA


1. Baragumu litalia, ndipo watu wa Mungu
Watakapokusanyika mbinguni.
Watakaribishwa kwake kwa furaha na
shangwe, Utakuwa mkutano wa pekee.


Tutamwona Yesu na watakatifu wote
mbinguni. Tutamsifu Yesu aliyeangikwa
msalabani.


2. Na malaika wa Bwana. atatangaza
kwamba, Wakati wa neema umekwisha
Wateule wamekwenda kumlaki Mwokozi,
Utakuwa mkutano wa pekee.


3. Na wenye dhambi watakaoachwa
Duniani. Watapata taabu na dhiki kuu,
Bali Bibi-Arusi ataingia mbinguni.
Utakuwa mkutano wa pekee.


4. Na malaika wa Bwana watakapotangaza,
“Ni mwaka wa Yubile wa milele”, Wateule
wataimba sifa za Mwana-Kondoo.
Utakuwa mkutano wa pekee.


Comments