71 EE RAFIKI SHAKA ZAKO


  1. Ee Rafiki, shaka zako Zipeleke kwa Yesu!
    Anayemwamini Yeye, Hata tahayarika.


    Namwamini, namwamini, Namwamini Mwokozi.
    Naamini, naamini Neno lake la kweli.



  2. Ziungame dhambi zako Utakaswe kwa
    damu! Akuvike haki yake, Akufikishe kwake.


  3. Masumbuko yako yote Uyaweke kwa
    Yesu! Akuvike haki yake, Akufikishe kwake.


  4. Na furaha yako pia Ijulikane kwake.
    Ndiye Bwana juu ya yote, Anayekubariki


  5. Tena mpe Bwana Yesu Roho, nafsi na mwili!
    Vyote vya maisha yako Yeye avitakase.

Comments