73 NAIFAHAMU NJIA


1. Naifahamu njia ya kwenda mbinguni, Ingawa
inapita kwenye majaribu. Bali yanifikisha mjini
huko juu, Na njia ni Yesu na njia ni Yesu.


2. Najua amani iliyo ya milele, huwezi kuipata kwa
mali yo yote. Ni tunu ya rehema kutoka kwa
Baba, Amani ni Yesu, Amani ni Yesu.


3. Najua kuna nguvu ya kuponya roho, Iletayo
amani faraja na raha. Inanilinda vema na mavazi
safi, Na nguvu ni Yesu na nguvu ni Yesu.


4. Najua na kifiko, ni huko mbinguni, Na siku ya
kufika inakaribia. Yafaa kukaza mwendo kupiga
mbio tu! Kifiko mbinguni, kifiko mbinguni.


Comments