1. Mimi ni m-geni hapa duniani, Nyumbani ni
mbali huko mbinguni juu. Mimi ni mjumbe
kutoka kwa Mungu, Nina habari ya mfalme.
Habari yake nzuri sana, Furaha ya
malaika: “Mpatanishwe na Mungu Baba
yetu!” Ndio ujumbe wa mfalme!
2. Mwokozi asema na kila m-moja: Urudi kwa
Baba kutoka utumwa! Ufike kwa Yesu na
dhambi utubu! Ndio ujumbe wa mfalme!
3. Mbinguni huko juu, vyote vya ajabu, Kuna
furaha kuu na raha milele. Umwamini Yesu,
atakufikisha. Ndio ujumbe wa mfalme!
Comments
Post a Comment