75 MIMI NI MSAFIRI


1. Mimi ni msafiri, mgeni duniani; Si kwangu hapa
chini Ni huko mbinguni Ninatamani sana kuka-a
daima Pamoja na Babangu kwenye utukufu.


Sijaona hapa mahali pazuri
Kama huko mbinguni.


2. Mwokozi yuko huko, Rafiki yangu mkuu,
Aliyenikomboa na kutoa dhambi. Na hata
nikiona furaha daima, Ningali natamani makao
mbinguni.


3. Na hata nikipewa vitu vya thamani, Na
kuimbiwa nyimbo za kufurahisha, Rafiki zangu
wote wakinipendeza, Ningali natamani makao mbinguni.


4. Upesi nitaona kifiko mbinguni. Mwokozi
wangu Yesu anikaribisha; Na huko nitaona
nilivyotamani, Kinubi nitapiga kumsifu Mwokozi.


Comments