76 MIMI MGENI, NINASAFIRI


1. Mimi mgeni, ninasafiri, Siku chache,
Naishi huku chini. Sitazuiwa kuwafuata,
Watakatifu walioshinda!
:/: Mimi mgeni, ninasafiri, Siku chache naishi huku chini.: /:


2. Nimo njiani, napiga mbio, Sina budi
Kukaza mwendo wangu, Na mkononi
Natwaa gongo, Nazo silaha nimejivika.
:/: Nimo njiani, napiga mbio,
Sina budi kukaza mwendo wangu.:/:


3. Ulimwenguni sioni raha, Natamani
kuingia mbinguni. Machozi, kufa,
maombolezo, Sitayaona mbinguni kamwe.
:/: Ulimwenguni sioni raha, Natamani
Kuingia mbinguni.:/:


4. Mchunga mwema, ninakuomba:
“Tangulia, uniongoze njia. Kwa kuwa yule
Mkuu wa giza, Aniwekea mitego mingi!
:/: Mchunga mwema, ninakuomba: “Tangulia, uniongoze njia!”


Comments