1. Kazi ni yako Bwanangu tunayoifanya.
Hakuna anayeweza kuvunja kazi hii.
Ni kama punje ya mbegu, Ikiwa ndani
ya mcha-nga. Inakufa kwa kuoza, Na
hapo yabadilika, Inaota, yakua na kuzaa.
2. Yesu umeteswa kwanza, halafu umepaa.
Nao wakufuatao wanateswa vivyo.
Twaomba tusaidie, Nasi tushike njia hii,
Kwa kufa kwako na sisi, Twatoka
kaburini,Tuongoze, tufike mbinguni.
3. Bwana wewe umekufa, Kwa ajili yetu,
Ukaweka ufufuo ulipofufuka,Twaomba:
Tuma mitume, Wajulishe jina lako,
Mpaka mwisho wa dunia! Utukubali na
sisi, Kwa kazi hii, tutume twakutii!
Comments
Post a Comment