1. Ninao uzima tele, Tumaini la milele, Na
mbinguni nitamwona Bwana Yesu kwa furaha
2. Ninao urithi bora, Unaotunzwa mbinguni
Hata nikijaribiwa Natiwa nguvu na Baba
3. Namshukuru Mungu wangu, Anitunza kila siku.
Katika shida na taabu Wala sisumbuki tena.
4. Nina amani rohoni, Ninaimba kwa furaha,
Nikiongozwa na Yesu Naendelea salama.
5. Ee Bwana, unifundishe Nikutumikie vema
Wakati unaobaki Kwa kuishi duniani.
Comments
Post a Comment