79 MAISHA YA MTU HAPA DUNIANI


1. Maisha ya mtu hapa duniani, Ni kama kusafiri
baharini. Twavuka bahari katika hatari,
Ni vema tukiwa na Kiongozi.


Ikiwa Mwokozi anatuongoza Twaona
Amani na raha kweli. Atatufikisha salama
mbinguni, Humo hatutakumbuka safari.


2. Twapita katika baridi na pepo, Maneno ya
Mungu ni nuru yetu. Hatari na hofu na chombo
kibaya, Tukiwa na Yesu hatuogopi.


3. Ingawa mawimbi yapiga kwa nguvu,
Tunavumilia mpaka mwisho. Na huko hakuna
dhoruba na pepo; Safari tutamaliza salama.


4. Tutakapofika bandari ya mbingu Tutamshukuru
Mwokozi mkuu. Hatutaziona hatari na hofu
Karibu na Yesu, Mwokozi wetu.


Comments