80 ZITAKAPOTIMIA SIKU ZA KAZI


1. Zitakapotimia siku za kazi yangu,
’taona asubuhi ya uzima. Mbinguni huko
juu nitamwona Bwana Yesu,
Ndiye atakayenikaribisha.


Nitamwona, nitamjua, Na karibu na
Yesu nitakaa, Nitamwona, nitamjua,
Kwa alama mikononi mwake.


2. Itakuwa furaha kuona uso wake
Na uzuri wake wa kupendeza,
Moyo utafurika kwa furaha na heri,
Ju-u ya kao aliloliandaa.


3. Na walio mbinguni waningojea huko,
Ninakumbuka tulipoachana.
Wataimba kabisa na kunikaribisha
Ninapenda kwanza kumwona Yesu.


Comments