81 ALIPOKUFA BWANA YESU


1. Alipokufa Bwana Yesu m-salabani
Akaishinda dhambi, uwezo wa Shetani,
Aliniweka huru, nifunguliwe kweli,
Nitakwenda mbinguni kwake juu.


Kule niendako Uchafu haupo, Ni nchi nzuri ya
salama kuu. Bwana Mungu wetu, Atuangazia,
Ee ndugu, tuonane huko juu!


2. Ninaifuata njia ya Mwokozi wangu,
Aniongoza vema, anifuta machozi.
Ananilinda katika hatari njiani,
Kwa Yesu Kristo vita yaisha.


3. Mbinguni nchi yangu, bendera ni upendo,
Roho ndiye arabuni ya urithi wangu.
Neno lake ni chakula changu safarini;
Neema yake itanifikisha.


Comments