82 NAJUA NCHI NZURI


1. Najua nchi nzuri, Huko Mungu alifanya,
Nyumba na kao letu; Natamani kufika.


Mbinguni, Kao la malaika! Mbinguni, Vyote
vyametameta! Mbinguni, Mungu atualika,
Tukusanyike mbinguni juu!


2. Kati’ safari yangu Ninajiuliza hivi:
“Je, nami nitafika Penye nuru ajabu?”


3. Kwa neema ya Mungu Nami nitakaa
Kwake juu Na taji ya uzima Mwokozi atanipa.


4. Sasa napiga mbio, Nifike nchi hiyo
Ya uzima na shangwe, Niliyoitamani.


Comments