1. Ninajua nchi huko juu, Hapo Mungu
alijenga mji. Naye amwita mmoja
mmoja, Waliomaliza mwendo huku.
Shida na huzuni Hazitakuwako huko.
Yesu ayafuta machozi; Tutam – shangilia
Mwokozi.
2. Mbinguni hawataingia, wenye dhambi
wasiosafishwa, Rafiki ujihoji leo Kama u
tayari kuingia!
3. Tazama, mto ungaliko, Unaweza
kusafishwa dhambi! Ukaoshwe katika
damu, Ya Mwokozi wetu Yesu Kristo.
4. Nafurahi kwani najua Kao langu liko
huko juu. Natamani sana kufika.
Njoo, upesi Yesu, unitwae!
Comments
Post a Comment