86 TUTAONA FURAHA MBINGUNI


1. Tutaona Furaha mbinguni, Na makao ya
watu heri. Tutakuwa pamoja na Mungu
Na kumsifu Mkombozi.


Tutafurahi na tutaabudu mbinguni kwa
Mungu Bab. Tutafurahi na tutaabudu
Tutakapofika juu.


2. Mara nyingi furaha hapa
Yageuka kuwa huzuni, Kwa Mwokozi
hazitakuwako Sikitiko wala shida.


3. Kama shida na shaka zafika
Kuzuia safari yetu, Tutazame mbinguni
daima, Raha yetu ni huko juu.


Comments