1. Mponyaji yupo hapa, Yesu wa neema
kubwa. Twapata uzima wake, Tumsikie Yesu!
Mbinguni na hapa chini Jina lake ndilo
Zuri. Yesu wa neema kuu, Yesu wa upendo.
2. Asamehe watu dhambi Wakizitubu kwake.
Awapokea kwa neema, Awapa afya nzuri.
3. Tukiwa na sikitiko, Yesu atufariji.
Tukiwa naye karibu, Hatuogopi kitu.
4. Watoto wapenda sana Kumwita Bwana
Yesu, Awashindia mabaya, Na majaribu yote.
5. Shetani anaogopa Jina la Bwana Yesu.
Katika vita ya dhambi, Anatutia nguvu.
6. Mbinguni juu kwa Furaha Tutamwona Bwana.
Shida zote zitakwisha, Tutamshukuru Yesu.
Comments
Post a Comment