- Cha kutumaini sina, Ila damu yake Bwana.
Sina wema wa kutosha, Dhambi zangu kuziosha
Kwake Yesu nasimama, Ndiye Mwamba
ni salama, Ndiye Mwamba ni salama. - Njia yangu iwe ndefu, Yeye hunipa wokovu.
Mawimbi yakinipiga, Nguvu zake ndiyo nanga. - Damu yake na sadaka, Nategemea daima.
Yote chini yakiisha, Mwokozi atanitosha. - Nikiitwa hukumuni, Rohoni nina amani.
Nikivikwa haki yake, Sina hofu mbele zake.
Comments
Post a Comment