90 YESU, YESU, JINA ZURI


1. Yesu, Yesu, Jina zuri, Wimbo wa malaika!
:/:Limekuwa ndani yangu Mto wa furaha tele.:/:


2. Jina lake kama nyota Lanionyesha njia.
:/:Kati’ majaribu yote Na shida ulimwenguni.:/:


3. Ni mikono ya upendo Ya kunikumbatia.
:/:Hapo ninalindwa vema Kama chombo bandarini:/:


4. Jina la Yesu Mwokozi, Ni wimbo safarini!
:/:Linaniletea raha, Toka nchi ya mbinguni:/:


Comments