91 YESU, JINA HILI JEMA


1. Yesu, jina hili jema Lichukue daima!
Lina raha na faraja Uwe nalo po pote!


Jina la Mwokozi, Lina matumaini!
Jina la Mwokozi, Jina hili ni Yesu!


2. Lichukue jina hilo Lenye nguvu kushinda!
Ukijaribiwa huku Taja jina la Yesu!


3. Yesu, Jina jema sana, Latutia shangwe kuu;
Kimbilio tena ngome, M-saada kwa wote.


4. Kila goti litakunjwa Mbele ya Bwana Yesu,
Watu wote watakiri, Kwamba Yesu ni Bwana.


Comments