92 YESU! JINA HILI


1. Yesu! Jina hili linapita Kila jina
ulimwenguni.Yesu, Yesu! Jina hilo
limetuletea wokovu.


Jina la Yesu ni lenye nguvu
Ya kuondoa dhambi zangu. Yesu, Yesu!
Jina hilo, Lanipa furaha na shangwe.


2. Hakuna jina kama la Yesu Lenye uzima
na uwezo. Yesu, Yesu! Jina hilo Malaika
wanalisifu.


3. Jina hili lina wema mno Linasujudiwa
mbinguni. Yesu, Yesu! Jina hillo,
Linaimbiwa duniani.


4. Sitaweza kumsahau Yesu Kwa kuwa
aliniokoa.Yesu, Yesu! Nitamwona Huko
mbinguni kwa furaha.


Comments