93 SIKU CHACHE TENA WAKRISTO


1. Siku chache na tena wakristo Watakwenda
kumwona Yesu. Siku chache na wataipewa
Thawabu taji ya uzima.


Nangoja sana Bwana Yesu Atakaporudi toka
mbinguni. :/:Kwa dalili zote ninaona sasa
Kwamba Yesu yu karibu kurudi. :/:


2. Siku chache za vita huku, Tena
Yesu Mfalme aja. Tutaona furaha
na raha, Atatupeleka kwake juu.


3. Siku chache na tena machozi, Yatafutwa
na Bwana Yesu. Na baada ya siku si
nyingi Nitaingia mbinguni juu.


4. Siku chache na tutasikia Baragumu
lake la mwisho. Waaminifu watachukuliwa,
Kukaa pamoja na Yesu.


Comments