1. Sasa kumepambazuka, Vivuli vya usiku
vinakimbia; Waulizwa, U tayari? Yesu atarudi!
Na kama upepo uvumavyo pote,
Injili ipelekwe kwa watu wote. Neno la
furaha na matumaini; Yesu atarudi!
2. Watu wengi wamefungwa Katika
Utumwa wa dhambi na giza.
Uhuru ni kwa Yesu tu, Naye atarudi!
3. Wanadamu wanaamka,
Nuru ya Injili yafukuza giza.
Tutapelekwa mbinguni, Yesu atarudi!
Comments
Post a Comment