1. Nchi nzuri ya ahadi yatungoja huko juu,
Watakapokusanyika wakristo.
Siku zinazobakia zinapita upesi,
Waaminifu watairithi nchi.
Lo! Ufalme wa Mungu u karibu! Lo!
Ufalme wa Mungu u karibu!
Niwe safi rohoni na kukesha daima,
Bwana Yesu yu karibu kurudi!
2. Twaamini kwamba tutaiona nchi ile,
Tunam-ngojea Mwokozi wetu.
Kwa dalili tunaona siku yakaribia;
Bwana Yesu yu karibu kurudi!
3. Maandiko yasema: Mkombozi atakuja,
Katika mawingu atatokea.
Haleluya! Bwana Yesu atamfunga
Shetani, Aliyejaribu kutupoteza.
4. Katika kum-ngoja Yesu wengi
wamechoka, Waamshe, uwaonye kwa
bidii. Kwani Neno la Mungu linatimizwa
upesi, Kwamba Yesu yu karibu kurudi!
Comments
Post a Comment