1. Mwokozi wetu aliahidi Ya kwamba
atakuja siku moja Kutupeleka mbinguni
kwake, Yawezekana hata leo.
Sioni shaka, Nina imani Kwa Mkombozi
Na damu yake, Na Roho wake Mtakatifu,
Ni arabuni ya urithi.
2. Wajumbe wengi wa Bwana Mungu,
Watumwa sasa duniani pote.Waitangaza
habari njema. Ya Yesu na pendo lake kuu.
3. Na watu wengi wanaamini,Wanaitika
mwito wa Mwokozi. Kwa roho moja
twakaza mwendo. Tuifikilie thawabu.
4. Twakaribia wakati ule Wa kuja kwake
Bwana Yesu Kristo. Na tujiweke tayari
wote Kuchukuliwa mbinguni juu.
Comments
Post a Comment