98 SIKU MOJA TUTAONA UTUKUFU


1. Siku moja tutaona utukufu wa Yesu,
Kama nuru ya umeme Yeye atatokea.


Uhubiri Neno lake kwa bidii po pote!
Siku ni karibu sasa, Bwana Yesu yuaja.


2. Tangu kale tumengoja siku ya ukombozi.
Hata nguvu ya mauti itaisha kabisa.


3. Ni uheri kwa wakristo kumlaki Bwana Yesu.
Wamevikwa nguo safi kwenda naye mbinguni.


4. Upashe habari njema uwaponye wagonjwa.
Uokoe wapotevu! Nenda, usikawie!


5. Kwa dalili tunaona wakati u karibu,
Na mfalme atakuja kutupeleka kwake.


Comments