1. Siku moja nitamwona Bwana Yesu Mwokozi.
Na milele kwa furaha Tutakuwa pamoja.
Nitam-tazama Yesu, Katika utukufu.
Huko kwa ukamilifu Yote nitafahamu.
2. Wema wake naujua Hapa kwa sehemu tu,
Huko nitamwona kweli, Na kushibishwa naye.
3. Shangwe gani kwa Mwokozi! Shida zote zaisha,
Giza halitakuwako, Huzuni itakoma.
4. Yesu yuaja upesi, Mwenyewe atashuka!
Tutanyakuliwa juu, Ili kumlaki Bwana.
Comments
Post a Comment